Powered by Blogger.

Search This Blog

Dalili za uchumba mbaya na usiofaa



Hizi ni dalili mbaya ambao hazitakiwi kuwepo kwa wachumba , ambazo unapoziona katika mahusiano yako jua inawezekana kabisa ndoa yenu isiwe na furaha kabisa.

1. Uchumba unaanza kwa kutaka ngono kutoka kwa mwingine, epuka ngono katika uchumba , na ukiona mtu ambaye anataka ngono ndo uchumba uendelee mwepuke.

2.Ugomvi
Uchumba ambao kila baada ya wiki ni ugomvi  si uchumba mzuri sasa kama katika uchumba mnagombana unategemea mini katika ndoa?

3. Tamaa
Uchumba ambayo mvulana au msichana anataka zawadi kila Mara kutoka kwa mwenzake na asipipewa ananuna na anatishia asipopewa anavunja uchumba .

4.gizani.
Uchumba wa ninyi kukaa gizani au Massa ya gizani mkiwa ninyi wawili tu, na usiku mnatumia muda mrefu sana hata usiku wa manane. Uchumba huo haufai." Mazoea ya kukaa mpaka usiku wa manane ni mazoea mabaya. Na hayampendezi Mungu hata kama ninyi wote ni wakristo .Massa haya yasiyofaa yanaathiri afya ,yanaifanya akili isifae kwa majukumu ya siku inayofuata, na yanakuwa na mwelekeo wa uovu."

5.Uchumba ambao unapokwazwa na mwenzako unachukua uamuzi wa kunywa sumu au kujinyonga, huo ni uchumba mbaya.

6.uchumba ambao kila siku unashawishiwa tu kila siku ili uchumba uendelee,na kudumu,maana kuna kughairi kwingi.

7.uchumba wenye wachumba wengi kiasi kwamba huchagua yupi lakino wrote wanamatumaini kwako huo sio uchumba .

8.uchumba bao hamtaki kutambulishana kwa wazazi wala ndugu na hata waumini wenzenu.unakuwa uchumba wa kificho,huo haufai.

Zingatia haya unapoyaona katika uchumba wako kuwa macho na chukua hatua.
Kama unaswali au kujua mengi zaidi.
Install App ya upendo wa kweli kutoka play store. Ni bure kabisa.

3 comments:

  1. Mimi nina mchumba wangu kila siku ana zungumzia mambo ya ngono na vurugo kila saa ila niko mbali naye saana

    ReplyDelete
  2. Mimi ninamke ila tulianza na mapenzi ndio tukaoana

    ReplyDelete