Powered by Blogger.

Search This Blog

Madhara ya tendo la ndoa kabla ya ndoa



Habari za wakati huu mpendwa msomaji na mfatiliaji was vipindi vyetu,
Siku ya Leo naona furaha kukuandikia kuhusu somo hili LA muhimu sana katika masuala ya mahusiano.
Akili yangu imesumbuka sana kuhusu hili kwani kuna matatizo mengi ambayo yanatokea katika mahusiano ila sababu kubwa, ni suala la kufanya mapenzi kabla ya ndoa,

Wengine najua wanaweza kutetea halo hii kwamba haiwezekani kuwa na mtu alafu usimjue kimwili, ila hakuna MTU hata mmoja mwenye sababu za msingi.

Maana bila kuangalia wewe unasali dini gani ila dini nzozifahamu hada wanaomwamini Mungu wa mbinguni hakuna sehemu hats moja inayoruhusu tendo la ndoa kabla ya ndoa.

Ila kuna watu wamekuwa na msemo kuwa siwezi kuuziwa mbuzi katika gunia cha ajabu hata wasichana nao wanakuwa na wazo hili ambao tendo la ndoa Luna waathiri sana kuliko wanaume.
Hili hatuna budi kuliangalia kwa unakini.

Tendo la ndoa lipo kws ajili ya wanandoa kwani ndicho kiunganisho cha mwili was mwanamke na mwanaume,
Kwani tunajua fika kuwa ,mwanaume atamwacha baba yake na mwanamke atamwacha baba na mama yake ataunganika na mume wake nao watakuwa mwili mmoja. Hawaunganiki kwa kula pamoja! Wala kumfulia nguo Bali kwa tendo la ndoa, sasa we we unayeruhusu kulala na mwanamke au mwanaume je, umewaacha was kwenu ? Au bado unatoka kwenu na kujiiba?

Ebu tuangalie madhara ya kufanya tendo la ndoa kabla ya wakati.

Kuharibu uhusiano na Mungu.
Tunajua kuwa mahusiano yetu yanatakiwa yaongozwe na Mungu ili yawe imara hata katika uchumba na ndoa, ila mnapoanza katika kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa basi mnamfukuza Mungu nankubaki na shetani, kwani mmevuja agano lake na miili yenu.

2 . kupunguza uaminifu.
Sababu kubwa mojawapo ya kuyumba kwa mahusiano ni kukosa uaminifu katika mahusiano sasa kulala na mtu kabla ya ndoa, yeye mwenyewe kwanza hatakuamini, maana anajua kabisa nikosa na amekushawishi ukakubali sasa je, mwingine akikushawishi si utakubali? Na hilo limeluwa tatizo linaloendelea hata katika ndoa ukikubali kulala na mwanaume Hugo sasa hivi kwa kigezo cha kulinda uchumba wenu ujue hatakuamini milele hata kama akikuoa maana ile alama ya were kumkubalia itarudi kichwani kuwa so mwingine anaweza kunywea kisima changu? Na ukikataa mpaka ndoa, akikuoa atakuamini sana hatakuwa na mashaka na wewe kwani anajua kuwa wewe so mwepesi kushawishika na mwanaume.

3.kuachika au kuvunjika kwa mahusiano sababu kubwa ya kuvunjika kwa mahusiano ni kufanya ngono. Kivipi.
Mwanaume ngono ni kama starehe kwake ila.mwanamke ni upendo au ishara ya Upendo. Mwanaume anamataka mwanamke kingono ili kuridhisha tamaa sake za mwili ila mwanamke anakubali kulala na mwanaume kama ishara yabupendo na hapo ndoa mambo yanapochanganyana.
Mwanaume akilala na wewe ni rahisi sana kukuacha, kwasababu mbili. Moja hakuna asichokijua kuhusu wewe mwili wako wore kaufunua amekumaliza so hana hamu na wewe hivyo atamtafuta mwingine na wewe utaachwa kimya kimya. Na hwenda hakuna unachokijua isipokuwa kutoa ngono tu.
Pili atakuacha kwasababu kiukweli hata mwanaume wengi hawapendi kuoa msichana ambaye no mwepesi sana kutia ngono. So ataona tatizo katika ndoa na hivyo atakuacha akitafuta aliye pure.


4.hupunguza heshima katika jamii.
 tendo hili si jema hata kidogo kulifanyabkwa watu ambao si wanandoa hivyo hata jamii itakupunguzia heshima japokuwa linaanza kuonekana kama suala la kawaida ila si kawaida. Zinaa imeeenea.
.
Wadada wengi sana wanalia kuachwa kwasabu walitoa mwili was kwa huyo jamaa na mwisho anaachwa na hivyo wengine hutaka kufa, ila chanzo no ngono maana umempa kila kitu katika moyo na mwili wako sasa anapokuacha unaona kama huna chochote ambacho ni cha heshima na unaamua kufa. Pole sana tambua kosa lako. Linda mwili wako sana tambua unapomvulia mvulana unapunguza asilimia za Upendo na jiandae kuachwa muda wowote.

Naumia sana napowaona wadada wanajirahisi kwa wavulana wanjipeleka kama ngombe anayepelekwa machinjioni ila hawajui kile kitakachotokea baadae.
Tambua kuna mambo ambayo sijaandika kama mimba ,UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa. Ila nakuoma Dada yangu sana na kwahuruma sana, Linda mwili wako usiruhusu hatabkama unampenda vipi,Linda hishima yako, hakuna mwanaume aliyekamilika ambaye akinyimwa ngono atakufa,
Tunza mwili wako.

Na kaka yangu nakuomba pia Linda mwili wako, Hugo binti hatokuamini ,ila pia jua hata Mungu umemkosea  .
Ngono unaweza kusamehewa dhambi hivyo ila madhara yake yatabaki milele daima, hivyo hata ndoa yenu kuna uwezeknao mhimiri wake akawa shetani.
Tunza mwili wako.
Naandika hata kwa uchungu sana maana ,naona wadada wakijiangamiza wenyewe,
Jiandae kutarikiwa au kokosa amani katika ndoa.
Huo ni ushauri unaweza kuendelea kufanya tu. Ila mie nimekwambia tena kwa Upendo ,
Asante kwa kuinstall App ya upendo was kweli.

8 comments: