Powered by Blogger.

Search This Blog

Unafanyaje ndoa inapoingia katika migogoro?


Hata uwe mwema vipi , changamoto zinaweza kutokea, na hivyo ukiona mtu ndoa yake inashida hivyo usimcheke Bali mwombee. Na msaada zaidi,

Na kama kuna tatizo, unaweza kuwaona washauri katika kutatua, ila Wa kwanza ni Mungu maana Bwana asipoijenga nyumba akeshaye akesha bure,

Na changamoto zinapotokea usiogope wala kukata tamaa katika ndoa yako.

1.Tafuta kujua chanzo cha tatizo lililo katika ndoa yako. Mfano kama mume amekutukana au kutoka nje ya ndoa, basi jiulize kwanini, na kwanini mpaka update chanzo msingi cha tatizo hill.

2.Jiulize mchango wako ni mini kwenye hilo tatizo.
Mnapokuwa wawili inawezekana kuhusima katika sehemu moja au ndog, yawezekana kuna kitu hujakifanya sawasawa. Je, uko tayar kukili? Mfano kama wewe unahusika katika hilo, na kukili kunaweza kutatua tatizo kwa kiwango Fulani.

3.Tafuta muda mwafaka Wa kuzungumza matatizo, si kila wakati, na pia usisubiri tatizo lako liwe kubwa ,

4.Chagua vita yako, kuna vitu vingine ni vya kuachia tu au kupotezea si kila kitu kiwe ugomvi, kwa hiyo angalia hilo, mfano kusahau vyombo, kusahau soks sebuleni, nk.

5.Usitumie vitisho.
Kama ni hivyo naona tuachane au maneno kama hayo, maneno ya vitisho ni ishara kuwa hujajiandaa kuingia kwenye ndoa, kama hauko tayari bora usioe, komaa kwanza.

6.Usimseme vibaya vibaya mke. Wako au Mme wako kwa watu wengine hasa wale ambao hawawezi kukusaida, wakati unapokuwa katika wakati,mgumu,
Usiwagombanishe watoto na mzazi . Waepushe watoto na ugomvi wenu.


7.Omba ushauri Wa kitaalamu, kwa watu wanaohusika. Wale ambao wanajua maadili ya kishauri, wasiotoa siri nje.
Dumu kuwa mkristo, hats katika kipindi kigumu.


8.ukipata nafasi ya kuongea , usikumbushie mambo ya zamani.

9.Omba Mungu, kibinadamu haiwezekani, Omba Mungu akusaidie usijenge chuki kwa huyo aliyekukosea, unaweza kupata matatizo ya kiafya kwasababu ya misongo, ukakosa kula. Usife kwasababu ya mwanaume Omba Mungu kusaidie na akupe moyo , ukifa yeye anaendelea kuishi na ataoa na kuishi vema tens kwa furaha.

10. Usiache kujifunza kwasababu ya changamoto za ndoa, endelea kula,kuoga,kusali na mambo mengine ya msingi.

Kupata mengi zaidi basi install App ya Upendo Wa kweli .
Pia fatilia video zetu YouTube kwa channel ya Upendo Wa kweli-original



No comments