Powered by Blogger.

Search This Blog

Namna ya kuomba msamaha kwa mpenzi wako

Katika mahusiano je neno kusamhe au msamaha unalichukuliaje? Unafikiri nini juu ya msamaha?

Kuna watu ambao kweli wanaudhi yaani kupenda kote unampatia kila kitu unampa mapenzi yako yote lakini bado anakutenda yasiyo paswa basi yaweza kuwa mara moja wwakati mwingine inajirudia.
Je kuna haja ya kusamehe kwa mtu ambaye anarudia makosa tena wakati mwingine kwa makusudi?

Leo tuangalie sehemu mbili za muhimu katika jambo hili
Tutaangalia pande mbili za msingi katika suala la kuomba msamaha au swala la msamaha katika mahusiano.

Kuomba msamaha
Katika sehemu hii kuna uhitaji wa kuelewa swala zima la kuomba msamaha kuna watu unakuta kweli kakosa na anakubali kukosa ila namna anyotumia kuomba msamaha siyo kabisa unakuta anashindwa kusamahewa si kwamba aliyemkosea hataki kumsamehe, lah bali yeye kaomba vibaya msamaha kwa mwenzi wake.
Kivipi?
Iko hivi , baadhi ya maneno hayafai kabisa katika kuomba msamaha kwa mwenzi ambaye umemkosea 
Epuka maneno haya.
Yaishe.
Neno hili wengi hulitumia hasa pale wanapokuwa wanaomba msamaha kwa wenzi wao , kwa kutaka mambo yasiwe magumu basi aliyekosea hutumia neno hili yaishe hii ni hatari kubwa sana katika mahusiano yenu. Cha msingi angalia namna mnavyoweza kualiza tofauti zenu bila kutumia neno hili "yaishe".

Potezea
Neno hili linafanana kwa ukaribu sana na meo yaishe kwa hili unamwambia asijali kwa kile ulichokosa hii huonesha kuwa hujutiinkosa lako na unataka achukulie poa.
Kaka yangu na dada yangu nikusihi jambo hili epuke maneno haya katika mahusiano bali tumia njia sahihi ya kuomba msamaha.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUOMBA MSAMAHA
Katika kuomba msamaha kuna mambo hakika yanahitaji huyazingatie tena kwa nguvu nasi mchezo ili kuponya mahusianobyako.
1
Angali mood ya mwenzi wako.
Wakati mpenzi wako ana hasira usiharakishe kuomba msamaha kwani unaweza kusababisha akakujibu tifauti na vile ambavyo angekujibu kama angekuwa katulia. Hivyo zingatia kufanya hivi, mfano imetikea mmekosana alafu mepnzi wako kakasirika sana , kafura, ni vema kunyamaza zaidi na kumwambia mpenzi naona nimekukosea ila ntakueleza ukweli wote sitakuficha kitu,  naomba tukae au tutulie tutaongea, ukiina bado kafula si kwamba wewe ndo uingize point zako mwache atulie, kama kuna chakula mpatie akikikataa wewe usijibu nyamaza kwanza ika uoneshe kuona uthamaninwake na roho ya utulive na kisha endelea.
Sasa inapitokea akatulia unaweza kumwita na ukaanza kumweleza huku ukiwa umemwangalia usoni ukionesha uaminifu wa kile unachokiongea .
Unapoongea ukiona anataka kuingea usimwambie tulia kwanza bali unaweza kumwacha aongee kisha anapomaliza endelea pale ulipoishia usianzie alipoishiabyeye, hii itampa nafasi ya kujua anatakiwa kukusikiliza kwanza. Na unapomaliza , msifie onesha yakuwa huoendinkumpoteza mtu kama yeye mkumbushe mipango mliyopanga na mwambie yakuwa unamhitaji, na utampenda tu hata kama mtakosana vipi na kisha mwambie kwa sauti ya upole kuwa unajutia kosa lako na unaomba msamaha na akusamehe kabisa ili uwe na amani kwa kuwa tangu mmekosana hauna amani kabisa kwa hiyo msamaha wake utakuwa furaha yako.
Kisha msikilize akianza kuongea juu ya makosa yote ambayo umewahi kumtendea we msikilize wala usiwe na haraka . anaweza katikati ya maongezi akasema kwa hili itakuwa ngumu kukusamehe wewe mwache aendelee kuongea taratibu akili yake itaanza kutulia na atakusamhe.
Sasa tuangakie kitu kingine cha muhimu.
Kosa kubwa
Kosa kubwa ambalo wengi hulifanya hasa wasichana katika kuomba msamaha ni hili
Hawaamini katika msamaha wa maneno unajua kunatifauti ya mwanaume kusamehe nabwanatofautiana kumbuka kuwa mwanaume siku zote yeye ana hulka ya kutunza vitu moyoni kwa hiyo si mwepesi sana wa kusema na kubadilika hii si kwa wote ika baadhi.
Anaweza kusema nimekusamehe akimaanisha kweli amekusamehe ila tambua yeye yeye siyo Mungu so bado akawa na mawazo juu ya lile kosa sasa wewe unapoambiwa kuwa umesamehewa basi wewe usisubiri aanze kuonesha yale mapenzi ya awali haraka. Wewe anza kuonwsha zaidi upendo wako. Endeleza mapenzi yako kwake , mtendee mema na usimkumbushe juu ya kile ulichomkosea

Kosa la pili ni kumkumbushakumbusha et umenisamehe? Sitakukosea tena wewe dada usikumbushe tulia endeleza mapenzi yenu.

Msamaha una nguvu ,
Post ijayo tutaangalia namna ya kusamehe na kuzuia kosa lisijirudie tena.
Usikose.
Kumbuka kuinstall Application yetu ya UPENDO WA KWELI kutoka play store ni free kabisa.
Pia tembelea channel yetu ya youtube  kwa jina la UPENDO WA KWELI.

No comments