Powered by Blogger.

Search This Blog

KWANINI WANAUME WANACHEPUKA KATIKA NDOA ZAO

Watu wengi ujiuliza kuwa mme wangu nampa kila kitu na hakuna jambo kasema namnyima au kuna mapungufu yeyote ila jambo la ajabu anatoka na mto wa kawaida , au mke kuchepuka je nini tatizo?

suala la kukosekana kwa uaminifu katika ndoa limekuwa jambo la kawaida katika jamii zetu na mwisho kupelekea maumivu makubwa katika ndoa na kusababisha talaka, magonjwa au vifo kwani kuna baadhi ya watu ambao wamekatisha maisha ya wenzi wao kwasababu ya wivu wa kimapenzi.

Tuangazie baadhi ya sababu

hakuna jambo ambalo linatokea lenyewe katika maisha ambalo haliko na kisababishi.

1.TABIA

Kuna watu ambao kwakweli wao ni kawaida kwao kuzoelea ngono na watu tofauti hivyo inakuwa ni tabia yao na kwasababu ni tabia yake basi tunajua kuwa tabia ni kama ngozi huwezi kuibadili hivyo hata akioa tabia yake ya kutokuwa mwaminbifu itaendelea tu mara nyingi na kusababisha maumivu kwa mwenzi mwingine. unaweza jiuliza je, nitajuaje? Rafiki mpenzi unaweza kujua hilo kama ukiwa makini kuchunguza katika maisha ya awali ya mtu huyo maana si rahsi mtu kubadilika mwenyewe kama halkuna nguvu ya Mungu ambayo immembadili katika hilo.


2.KUWA BUSY 

Baadhi ya wanandoa wamekuwa busy sana kiasi kwamba inakuwa bgumu kwa wengine kuweza kupata muda na wenzi wao, mfano unakuta mke yuko muda wote anawaa kazi hana muda wa kujua hali ya mume wake , hana muda wa kumuandalia chakula mume wake hana ,muda wa kucheka na mume wake, ujue kuna mtu atakutanana nae mahali ambae atampa pole kwa kazi atamsifia kwa kazi anavyozifanya katika ubora, na unajua kuwa mwanaume akisifiwa kuna ujambo linaingia katika akili yake kuwa mwanamke huyu anamthamini, hivyo inapelekea wao kuwa karibu zaidi hata kama yeye hakupanga kukusaliti ila wanaanza kuwa karibu zaidi na mwisho inapelekea kusalitiwa.

3.KUTOLIDHIKA KATIKA TENDO LA NDOA

Kuna wenzi ambao kinachowatoa nje ni kuwa wamefika mahali tendo la ndoa limekuwa kama jambo la kawaida haluna ubunifu sasa unakuta mwanaume anatoka nje tu ya ndoa , japo sababu ya msingi ni ujinga tu maana alitakiwa kusema wapi penye shida ili kuleta maboresho au kuwaona wahsauri, ila unakuta mwanamke ajishughulishi kitandani yeye ni kusubiri mwanaume aingize tu basi hakuna cha ziada, anasubiri mwanaume pale atakaposikia hamu basi hana muda wa kumtega mume wake sasa unakuta mume akifika mahali kama ofisini akakutana na kadada kakamvalia nguo za mitego yeye anaona mambo mapya na akili yake inaruka, kuangalia maungo ya mwanamke kwa mwanaume ni kama sumaku katika hisia zake hivyo anashawishika kusaliti ndoa yake bila kutarajia, RAI natoa rai kwa akina mama au wanawake au wasichana ambao mtaolewa jitahidi kumlinda mumeo na unawezaa kumlinda hivyo kwakuwa mbunifu ili aone kuwa wewe ni bora.

4.MAPISHI MABOVU

Wanawake wengine hawajuyi kupika na hawataki kupika au hawataki kujifunza kupika , unajua sisi wanaume ukweli tunapenda chakula kitamu hivyo mwanamke asipijua kupika na wala hataki kujifunza na kuboresha mapishi huwa ni changamoto. mfano unakuta mwanamke kaolewa na kila siku anayempikia mwanaume chakula ni dada wa kazi au mdogo wake mke (msichana) sasa kumbuka chakula ni kitamu na kila siku anayesifiwa ni msichana wa kazi na unajua unayemsifia sana unapenda zaidi ndo maana kumsifu Mungu hakumsaidii Mungu ila kunaongeza upendo na imani yetu kwake, so ukiacha mfanya kazi ndo atoe huduma za mapishi kwa mmeo jiandae atatoa huduma ya kitandani kwa mumeo pia maana ukishindwa madogo hata makubwa yatakushinda pia.

5.UKOSEFU WA HUDUMA MUHIMU

Mke unakuta huduma zote muhimu ndogondogo hufanyi kwa mumeo, kupeleka maji ya kuoga ni yeye mwenyewe au mfanya kazi, kunyoosha nguo yeye mwenyewe au mfanya kazi,kufua ni yeye mwenyewe au mfanya kazi, unadai unatafuta pesa unachokifanya ni tendo la ndoa tu mengine yote anafanya mtu mwingine unadhani mume alioa kwasababu ya ngono tu bila shaka hapana, anahitaji msaidia kimawazo kihisia na katika maisha kwa ujula kazi hakukuoa kwamba muda wako wote utumia kazin , toa huduma zote muhimu kwa mumeo .


ni MR GEE 0769558006 



No comments