Powered by Blogger.

Search This Blog

Lugha tano za Upendo.




Tunajua kuwa kuna lugha mbalimbali katika jamii au taifa.
Kama wewe umeolewa au umeoa jua kama humtunzi me wako wewe ni mbaya kuliko MTU asiyeamini .
Zipo njia katika katika kutunza.
1. Kutunza kiroho.
2.kutunza kimwili, mfano kuoga.
3.huduma ya kiuchumi
4.huduma ya kisaikolojia yaani kujua kuwa yuko vizuri au lah, unaweza kujua kwa kutazama tu, je umemsomajr mwenzi wako pale ambapo anakuwa sawa au lah. Sasa jua kwa uzuri namna jinsi alivyo.
Na yote haya yanafanyika kwasababu ya kitu kinaitwa Upendo, tambua Upendo ni uchaguzi wala so lazima.

Sasa ni vema kujiridhisha kuwa jinsi unavyopenda je ndivyo anapenda kupendwa? Unaweza kutumia juhudi nyingi katika kuonesha kwamba unampenda ila kumbe ni Bure.

Katika kupena tumia akili nyingi kuliko  nguvu nyingi, sasa je utafanyaje katika kuinesha kuwa unamtendea kile ambacho anpenda.
Sasa tuangalie lugha tank za namna ya kupenda.

Lugha lazima kueleweka , chagua lugha inayofaa katika kuonesha Upendo kwa hiyo mtu ambaye unampenda.
1.lugha ya kutia moyo. Kuongea maneno ya kutia moyo kwa mwenzi wako.ukiona MTU anasema huko busy sana ujue kuwa anadai kuwa humpi muda, na ukiona kuwa MTU anasema. Kama.anafanya vzuri basi ni vema kumsifia, maana kuna mwanaume wanapenda kusifiwa, mwambie wewe ni mwema,MTU mzuri, unaweza kuangaika kufanya mengi ila kumbe ziro, sasa usisahau lugha hii.
Kama anapika vizuri msifie kwa chakula kwa kitamu mpaka naing'ata ulimi.

2. Lugha ya kuwa na wakati mzuri.
Kuwa na muda naye , kufanya mambo mengi sana yanaweza yasionesha Upendo kuliko kutia muda Wa kukaa nae tu, mpe muda wako, mpige story, mambo mengi ya kutosha.

3.Kupokea Zawadi.
Kuna wengine wanapenda Zawadi, zaweza kuwa ndogo ndogo, ila marakwamara itakuwa poa sana, kufanya surprise za Mara kwa Mara, unaweza hats kuleta pipi, peremende na mambo mwingine kama hayo.

4.lugha ya usaidizi.
Kuna wengine wanapenda kusaidiwa yaani mfano anafanya kazi ukimsaidia anafurahi zaidi, tambua aina ya mwanamke uliyenaye, msaidie kazi,
Kuna mahali panapowashwa tumia akili katika kupenda.

5. Lugha ya kugusa.
Watu hawa wanapenda kuguswa, mfano wanapenda kukumbatia, au kubusu, watu Wa aina hii wanapenda ukae Katibu nao , ni poa sana. Angalia kama MTU Wa aina hiyo unaye akitaka kukugusa ukakataa ujue anaona kuwa unamkataa.

Wapendwa tambua lugha ya mke au mume wako, itakusaidia sana katika kudumisha Upendo wenu zaidi.
Mpende mtu kulingana na namna ambavyo anataka kupendwa wala hutateseka , kama hujui basi kaa nae, muulize Nate atakueleza kwa uzuri kabisa.

Kupata mengi zaidi install app ya Upendo Wa kweli kutoka play store utapata mengi zaidi.


No comments