Powered by Blogger.

Search This Blog

sababu ya mapenzi ya wanachuo wengi kutodumu


Kuna hali kubwa ambayo onaonekana na mengi nimekutana nayo katika mazingira yangu ya kusoma chuoni, na kusikia pia na watu wengi wakilia kuachwa au kupewa mimba na kutelekezwa wawapo chuoni na wenzi wao waliodhani wanawapenda sana kumbe sivyo.
leo tuangalie sababu kwanini mapenzi haya hayadumu sana ?
sababu iliyonyuma yake.

1. kuishi maisha ya kuigiza
wanachuo wengi hawaishi maisha yao yale ambayo yanatakiwa kuwa kwa hiyo wewe unamwona kuwa anafaa kumbe sivyo alivyo na hivyo inafikia kipindi ambacho hawezi kuigiza tena, na hivyo uhalisia unapoonekana mtu anashindwa kuendelea tena na maigizo na upendo lazima uingie doa.




2

.kutokuwepo kwa malengo
wanachuo wengine wanaiingia katika mahusiano bila kuwa na malengo, mfano umetokea kumpenda msichana fulani ni kweli wala siyo kosa ila je mnaingia kwenye mahusiano ili iweje?na mnategemea nini na mwisho wenu ni nini? kwahiyo kuwepo kwa malengo na commitment ni bora sana, msiishie kusema nakupenda nakumiss basi lazima kuwepo kwa malengo thabiti ya kudumisha mapenzi yenu.


3.Kutowajibika
wengi wanaingia katika mapenzi bila kujua wajibu wa mmoja mmoja ni upi na kuchukulia kuwa kawaida na mwisho wa mambo yote upendo unakosa ubunifu na kuishia kuanguka vibaya na kishindo kikubwa sana.
msichana hajui afanye nini na mvulana kadhalika kutokujua anatakiwa kufanya nini.

4.Mvuto na umaarufu
wengine pia wanaingia katika mahusiano na mtu kwasababu ni cute au mrembo sana au anavaa na kupendeza au chuoni ni msemaji na maarufu katika siasa au nyanja fulani kwa hiyo wala mtu hazingatii kipi ni bora katika mahusiano yao.
kumbuka mapenzi bora yanajengwa na mtu kuwa na moyo mwema na siyo sura tu,
na mwisho mtu huyo uliyempendea uzuri atachuja na utamwona wa kawaida pale uonapo mwingine.


5.kazi nyingi
ukweli ni kuwa unapokuwa chuoni kuna mambo mengi sana ambayo yanakukabili katika maisha na mitindo mingine ya maisha kiukweli,
mfano chuoni utakuta kuna assignment za kutosha, mitihani na kazi nyingi vikao,na mangine pia kumbuka kuna wakati ambapo mambo hayako sawa kimasomo unatafuta course work itimia kwa ajili ya mtihani wa mwisho(UE)
na kwa hivyo mapenzi kuwa katika hatari. na si hivyo tu bali una marafki na mambo mengine na hivyo kufanya mapenzi yenu kuwa hatarini.

No comments